Otile Brown aachana na mpenzi wake baada ya kuchumbiana kwa miaka 3

Muhtasari
  • Otile Brown ametangaza hayo kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram
  • Otile na Nabayet wamekuwa pamoja tangu 2018 baada ya Otile kuachana na Vera Sidika

Otile Brown ametangaza rasmi kuachana na mpenzi wake wa muda mrefu Nabayet, baada ya kuchumbiana kwa miaka mitatu.

Otile Brown ametangaza hayo kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram.

Otile na Nabayet wamekuwa pamoja tangu 2018 baada ya Otile kuachana na Vera Sidika.

Wamekuwa wakifanya mazoezi ya mapenzi ya umbali mrefu kwa sababu Nabayet alikuwa akiishi na kufanya kazi nchini Ethiopia.

Otile amesema yalikuwa makubaliano ya pande zote mbili na walikubaliana kwa pamoja kuachana.

Otile Brown sasa yuko single tena.

Otile Brown alithibitisha kwamba Nabayet alikuwa amewasili nchini ili kuzungumza kuhusu masuala yanayowakabili, lakini haikufaulu vyema.

“Mimi na Nabbi hatuko pamoja tena, mara ya mwisho tukiwa pamoja tulijaribu kutafuta njia ya kwenda mbele lakini tuliamua kuachana  kwa bahati mbaya....yeye ni mtu wa ajabu na kwa ajili ya hayo nitamheshimu milele na hata kumjali

Namtakia mema anapoendelea na maisha yake Ubarikiwe," Otile Aliandika.