Nabayet azungumza baada ya kutengana na Otile Brown

Muhtasari

•Nabii amejitokeza kwa mara ya kwanza na kuzungumza kwa mashabiki, akiwapongeza kwa kuwa naye kipindi hiki ambacho wameachana na mpenzi wake ambaye walichumbiana kwa miaka mitatu

• Nabii ameshukuru wote  ambao wamekuwa wakimtumia ujumbe wa kumjulia hali na kutaka kujua anavyoendelea na maisha yake baada ya kutengana na mpenzi wake Otile Brown.

Otile Brown na Nabayet
Otile Brown na Nabayet
Image: HISANI

Aliyekuwa mpenzi wa Otile Brown, Nabayet almaarufu Nabii amejitokeza kwa mara ya kwanza na kuzungumza kwa mashabiki baada ya mahusiano yao ya miaka mitatu kufika hatima.

Kupitia ukurusa wake wa Instagram Nabii ameshukuru wote  ambao wamekuwa wakimtumia jumbe wa kumjulia hali  baada ya kutengana na mpenzi wake Otile Brown.

"Asante kwa kuchukua muda wenyu kunijulia hali na kunitumia ujumbe wa heri ya maisha. Upendo wenyu ni wa ajabu sana. Naendelea vizuri," alisema mpenzi wa Otile Brown Nabii 

Siku ya Alhamisi Otile alitumia ukurusa wake wa  instagramu kutangaza kuachana na Nabii.

Ikumbukwe wapenzi hao wamekuwa kwenye mahusiano kwa tabribani miaka mitatu, baada ya Otile kuachana na aliyekuwa mpenzi wake mwanasoshailiti  Vera Sidika.