Mwanasiasa Rodgers Kipembe akwea Mlima Kenya kuombea Raila Odinga

Muhtasari

• Katibu mkuu wa chama cha NOPEU, Rodgers Kipembe amekwea mlima Kenya hadi kileleni kwa kile alichokisema ni ziara ya kumuombea Raila Odinga pamoja na Wakenya.

Mwanasiasa na Mfanyibiashara akiwa kileleni mwa mlima Kenya
Image: Rodgers Kipembe (Instagram)

Katibu mkuu wa chama cha NOPEU, Rodgers Kipembe amekwea mlima Kenya hadi kileleni kwa kile alichokisema ni ziara ya kumuombea Raila Odinga pamoja na Wakenya.

Kipembe ambaye ni mfanyabiashara na mwanasiasa wa chama cha NOPEU anasikika akielezea katika mkanda wa video kutoka kilele cha mlima Kenya kuwa wameenda kuombea Raila Odinga, kuwaombea wakenya ili wafunguke macvho wasidanganywe pamoja na kuombea chama chao cha NOPEU.

"Sasa, hapa tuko ni Lenana, sehemu ya juu kabisa ya mlima Kenya, na sasa hivi ni saa kumi na moja alfajiri. Tumekuja kwa huu mlima ili kupiha kitu inaitwa kambi ya maombi.

Tumekuja kuombea mtu anaitwa Raila Amollo Odinga," anasikika akisema kwenye video hiyo

Kipembe pia anasema wamelala barabarani na kukwea mlima kwani lengo lao ni kukwea mpaka Batiani kukita kambi wiki mzima ili kuombea wakenya wafunguke macho ili wasidanganywe na kufuata wezi.

"Kitu kingine katika ziara yetu hapa mlimani ni kuombea chama chetu cha NOPEU. Katika wiki hiyo moja hakuna kula wala kunywa," Kipembe anasema