Nay wa Mitego awashauri Watanzania kununulia Wema Sepetu Gari

Muhtasari

•Nay wa Mitego amejitokeza wazi na kueleza kuwa inafaa Watanzani wakuje pamoja wamchangie  muigizaji na mwanasosholaiti  Wema Sepetu wamnulie gari la kifahari kuomdolea machozi  yaliyomtoka siku ya Jumatatu

•Wema Sepetu alitiririkwa na machozi baada ya Aristostle kumdhalilisha mbele ya wafuasi wake kwamba ni muigazaji ambaye ni maarufu na cha kushangaza ni kuwa hana Gari

 

Wema Sepetu
Wema Sepetu
Image: HISANI

Rapa wa Tanzania Nay wa Mitego amejitokeza wazi na kueleza kuwa inafaa Watanzani waje pamoja wamchangie  muigizaji na mwanasosholaiti  Wema Sepetu wamnunulie gari la kifahari kumpanguza machozi  yaliyomtoka siku ya Jumatatu.

Wema Sepetu alitiririkwa na machozi baada ya Aristostle kumdhalilisha mbele ya wafuasi wake kwamba ni muigazaji ambaye ni maarufu na cha kushangaza ni kuwa hana Gari.

Kauli hii ya Aristotle ilikosolewa na wasanii wengi hasa  wajinsia ya kike wakisema Aristostle alidharau jinsia ya kike kwa jumla.

Nay wa Mitego kutokana na kile alikitaja kuwa ni kero kwa Wema Sepetu na Watanzania kwa jumla, amejitokeza na kushauri wa Tz  wamchangie muigizaji huyo angalau aweze kumiliki gari kama waigizaji sifika nchini humo.

"Kama kweli Wema Sepetu hana gari la kutembelea mimi naona tumchangie apate Gari zuri la kutembelea, Wema ameinspire mabinti wengi sana ambao kwa sasa wanaishi maishi poa," alisema Nay wa Mitego.

Wengine waliokerwa na maneno ya Aristotle ni Irene Uwoya ambaye ni mwandani wa Aristotle, Hamisa Mobeto na wasanii karibu wote wa Jinsia ya kike  kutoka Tanzania.