Zuchu aingia pango la 'Simba', atangaza siku ya kuasi ukapera

Muhtasari

•Ni takribani Miezi miwili imepita baada ya habari hizo, si kwa mitandao ya kijamii bali pia vyombo vya habari kama vile Radio na runinga kueneza uvumi kwamba wasanii hao wanchumbiana.

•Zuchu ameeleza kuwa siku hio kuwa maalum kwake ambapo anatarajiwa kuasi ukapera na kuwa na mke wa nguli wa Muziki wa Bongo Flavour Diamond Platnumz

 

Diamond Platnumz na Zuchu
Diamond Platnumz na Zuchu
Image: HISANI

 Ni bayana sasa yaliyokuwa yakifanywa gizani  yameanza kufichuka na kama wahenga walivyosema mapenzi ni kikozi hayafichiki.

Haya yameshuhudiwa kutokana na tetesi ambazo zimekuwa zikitamba kwenye mitandao ya kijamii kwamba  Diamond Platnumz anatoka kimapenzi na  Zuchu.

Ni takribani Miezi miwili imepita baada ya habari hizo, si kwa mitandao ya kijamii bali pia vyombo vya habari kama vile Radio na runinga kueneza uvumi kwamba wasanii hao wanchumbiana.

Kupitia meza ya udaku tumebaini siku ya 14 Februari itakuwa siku  ya ndovu kumla mwanawe ambapo kuna uvumi unasambaa kwenye mitandao ya Tanzania kwamba Diamond na Zuchu watafunga ndoa siku hio.

Kupitia ukurusa  wa Instagram, Zuchu ameeleza kuwa siku hio maalum kwake ambapo anatarajia kuasi ukapera na kuwa na mke wa nguli wa Muziki wa Bongo Flavour Diamond Platnumz.

Ikumbukwe siku ya Jumatatu,Mamake Zuchu, Khadija Kopa alizua madai kwamba Binti yake anatarajiwa kuolewa tarehe 14 Februari na anamuombea  mwanawe kutumia madili aliyompa wakati akikomaa.

Aidha, Mamake Diamond ameonekana kuwa na mtazamo tofauti na wale wanasema mwanawe anaoa siku ya Valentine Februari 14, huku akizua madai kwamba Diamond hajielewi ni kama amechanganywa na mazingaumbwe, ..."ni kama amerogwa"... Kauli ambayo inaonekana kama kutopendelea UhUsiano baina ya Zuchu na Simba.