Watu wengi hawachoki kupost ujinga-Anerlisa Muigai kwa wanaoingilia maisha yake

Muhtasari
  • Pia alowashauri mashabiki wake wanapaswa kuwachagua marafiki wao vyema iwapo wanataka kuishi maisha yenye furaha

Anerlisa aliachana na mpenzi wake msanii wa Tanzania Ben Sol na amekuwasigle tangu kuachan kwao.

Inavyoonekana, hakuna anayejua anachumbiana na nani kwwani amekuwwa akipakia picha na wanaume tofauti huku wengi wakishindwa haswa nani mpenzi wake.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amewaonya na kuwatupia makombora watu ambao hawalazi damu, bali wanapakia mambo ya watu kila kuchao kwenye mitandao ya kijamii.

Kulingana na Anerlisa inasikitisha sana kumuona mtu mwenye uwezo mkuwa wa kufanya jambo la maana akiharibu uwezo wake.

"Je baadhi ya watu hawachoki kupost vitu visivyo vya msingi mara kwa mara...anza kusoma kitabu jielimishe tafuta kazi na uifanye vizuri...chagua lughana kuikamilisha, kuhamasisha watu na kuwa na tamaa au tafuta hobby sio kufanya mambo ya kitoto kuanzia jumatatu hadi jumatatu.Mtu yeyote zaidi ya miaka 25 afanye hayo hapo juu..inauma sana kuona watu wenye uwezo mkubwa wanaenda ovyo," Aliandika Anerlisa.

Pia alowashauri mashabiki wake wanapaswa kuwachagua marafiki wao vyema iwapo wanataka kuishi maisha yenye furaha.