"Nakupenda dada!" Diamond amwandikia Esma Platnumz ujumbe mtamu kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa

Muhtasari

•Diamond alimwarifu dadake kuwa hangeweza kumpa zawadi yoyote ya siku ya kuzaliwa ila akaapa kumkabidhi mnamo siku ya Valentines

•Mama Dangote kwa upande wake alimtambulisha Esma kama rafiki wake wa dhati na kumtakia maisha marefu.

Esma Platnumz na Diamond Platnumz
Esma Platnumz na Diamond Platnumz
Image: HISANI

Siku ya Jumatano dada wa kambo wa mwanamuziki tajika Diamond Platnumz, Esma Khan alikuwa anaadhimisha siku yake ya kuzaliwa.

Esma ambaye ni mkubwa wake Diamond alimshukuru Maulana kwa kumjalia mwaka mwingine na kuoneka kupendezwa na ukuaji wake.

Marafiki, wanafamilia na wanamitandao walimmiminia malkia huyo jumbe kochokocho za kheri njema za siku ya kuzaliwa.

Diamond hakuachwa nyuma katika kumtakia dadake maadhimisho mema ya siku ya kuzaliwa huku akimhakikishia kuhusu mapenzi makubwa aliyo nayo kwake.

Nyota huyo wa Bongo ambaye kwa wakati huo alikuwa katika ziara nje ya Tanzania alimwarifu dadake kuwa hangeweza kumpa zawadi yoyote ya siku ya kuzaliwa ila akaapa kumkabidhi mnamo siku ya Valentines. 

"Siku maalum sana kwa dadangu  mpendwa Esma Platnumz. Nimeshindwa kukupa zawadi ya Birthday leo ila bado iko pale pale mnamo tarehe 14, Mlimani City nitakupatia..Nakupenda sana dada tena Mahaba Ndindindi" Diamond aliandika.

Mama Dangote kwa upande wake alimtambulisha Esma kama rafiki wake wa dhati na kumtakia maisha marefu.