Mercy Masika awashauri vijana kutocheza ngoma za unyumba kabla ya ndoa

Muhtasari

• Mwanamuziki, Mercy Masika amewarai  vijana ambao bado hawajafunga ndoa kujitenga na ngoma ya ndoa hadi watakapo ingia katika ndoa.

• Alieleza vijana kuwa popote watapokuwa  wakitembea  watakutana na watu  wanaovutia zaidi hivyo basi hio isiwe ni kizingizio cha kujamiana kiholela.

Msanii wa injili, Mercy Masika
Msanii wa injili, Mercy Masika
Image: instagram/mm

Mwanamuziki, Mercy Masika amewarai  vijana ambao bado hawajafunga ndoa kujitenga na ngoma ya ndoa hadi watakapo ingia katika ndoa.

Kupitia video aliyopakia kwenye ukurasa wake wa instagram  aliwashauri vijana kuwa ni vyema vizuri kuepukana na tendo la unyumba na ilhali hawako tayari kuanza familia.

Alieleza vijana kuwa popote watapokuwa  wakitembea  watakutana na watu  wanaovutia zaidi hivyo basi hio isiwe ni kizingizio cha kujamiana kiholela.

"Siku zote utapata watu wa kuvutia popote uendapo iwe umeoa au hujaolewa. Watu wa kuvutia watakuwepo kila wakati," alisema Mercy masika.

Isitoshe, alizungumza kuhusu wanandoa ambapo aliwashauri kuwa wajasiri na wavumilivu kwenye ndoa kwani anaelewa vyema ndoa sio jambo rahisi hasa  wakati huu wa karne ya ishirini na moja.

"Kuwa hodari na jasiri kwenye ndoa ni kukubali kuwa wewe ni mzuri...kuwa hodari katika maisha kama Mungu anavyotaka kutoka kwako," alieleza.