Msanii Juliani aonesha pete baada ya fununu za harusi

Muhtasari

• Msanii wa mtindo wa kufoka Julius Owino almaarufu Juliani ameonesha pete baada ya fununu za kufunga harusi na mpenzi wake Lillian Ng’ang’a

• Katika picha chache ambazo zimesambazwa kwenye mitandao ya kijamii, Juliani anaonekana akiwa na pete baada ya harusi hiyo ambayo minong’ono ya chini kwa chini inasema ilifanyika Februari 2.

Msanii Juliani akiwa na rafiki zake
Image: HISANI

Msanii wa mtindo wa kufoka Julius Owino almaarufu Juliani ameonesha pete baada ya fununu za kufunga harusi na mpenzi wake Lillian Ng’ang’a ambaye waliachana na gavana wa Machakos Alfred Mutua.

Katika picha chache ambazo zimesambazwa kwenye mitandao ya kijamii, Juliani anaonekana akiwa na pete baada ya harusi hiyo ambayo minong’ono ya chini kwa chini inasema ilifanyika Februari 2.

Ndoa hiyo inatajwa kuwahusisha watu chini ya hamsini huku hafla hiyo ikifanyika faraghani katika sehemu inayotajwa kuwa ni bustani ya Paradise huko Kiambu huku mapokezi ya harusi yenyewe yakifanyika katika mtaa wa kifahari wa Runda.

Katika picha hiyo, rafiki wa karibu wa Juliani ambaye pia ni mwanaharakati Boniface Mwangi anaonekana miongoni mwa marafiki wengine wa karibu na Juliani.

Mwangi katika siku za hivi karibuni wamekuwa wakizushiana maneno na gavana Mutua kwa kile anachodai gavana huyo anamwinda kwa sababu aliunga mkono mahusiano baina ya Juliani na Lillian.