Baadhi ya 'scandals' ni sisi wasanii utengeneza,'Willy Paul asema huku akiahidi mashabiki wake haya

Muhtasari
  • Wasanii wengi wanafahamika kutafuta kiki ili kibao chao kipya kiweze kuvuma na kupokea watazamji weni kwenye Youtube
Image: INSTAGRAM// WILLY PAUL

Msanii Willy Paul alifahamika sana baada ya kujitosa kwenye tasnia ya muziki, miaka 5 iliyopita, huku akifahamika sana mitandaoni kupitia kwa nyimbo zake.

Safari ya muziki ya msanii huyo haijakuwa rahisi kwani amekuwa akipokea kejeli mitandaoni, hii ni baada ya kuacha kuimba nyimbo za injili.

Licha ya hayo yote msanii huyo amekuwa akitia bidii kila kuchao, ili kuhakikisha mashabiki wake wameburudika.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram aliwaahidi mashabiki wake muziki mzuri mwaka huu, huku akidai kwamba baadi ya kashfa ambazo mashabiki uhuhudia mitandaoni ni wasanii huwa wanatengeneza wenyewe.

Wasanii wengi wanafahamika kutafuta kiki ili kibao chao kipya kiweze kuvuma na kupokea watazamji weni kwenye Youtube.

Hii ni moja wapo ya mbinu ambayo wasanii wengi hutumia katiika karne hii ya sasa.

"Hello fam, more music less scandals. Btw some of the scandals you see out there.. ni sisi wasanii utengeneza but this year expect nothing but good music..." Pozze Aliandika.

Kulingana na maoni yako je wasanii wanapaswa kutafuta kiki kwa ajili ya vibao vyao?