Zuchu aeleza sababu zake kuweka Wallpaper ya Diamond kwa simu yake

Muhtasari

•Malkia huyo wa muziki alisema kwamba Diamond sio bosi wake tu ila pia ni mtu muhimu sana kwake na ndiposa akachukua hatua ile.

•Zuchu alieleza kuwa Diamond sio mpenzi wake ila ni bosi wake katika lebo ya WCB.

Zuchu akana mahusiano ya kimapenzi na Diamond
Zuchu akana mahusiano ya kimapenzi na Diamond
Image: HISANI

Mwanamuziki mashuhuri kutoka Zanzibar Zuhuru Othman almaarufu kama Zuchu amekiri kuwa aliweka picha ya Diamond kama wallpaper kwenye simu yake.

Akizungumza na Wasafi Media, Zuchu alisema kwamba hakukuwa na sababu za kimapenzi kuweka Wallpaper ya Diamond.

Kwa msisimko mkubwa na tabasamu, malkia huyo wa muziki alisema kwamba Diamond sio bosi wake tu ila pia ni mtu muhimu sana kwake na ndiposa akachukua hatua ile.

"Yeye ni muhimu sana. Ni bosi wangu. Yeye ni muhimu tu" Zuchu alisema.

Haya yanajiri  huku uvumi kuhusu mahusiano yao ukiendelea kutanda. Wengi wamedai kuwa wasanii hao wawili wanapanga ndoa hivi karibuni.

Hivi majuzi Zuchu alieleza kuwa Diamond sio mpenzi wake ila ni bosi wake katika lebo ya WCB. Aliweka wazi kwamba tayari yuko kwenye mahusiano na jamaa mwingine anayempenda sana.

"Mimi sikai kwa Diamond. Kwa kweli nachumbiana na mtu, niko na boyfriend. Ni mtu tu wa kawaida. Ni mrefu kuliko mimi, ni maji ya kunde, ni mfanyibiashara na anafanya mazoezi. Siwezi kuwa na mtu ambaye hafanyi mazoezi, afya ni kila kitu" Zuchu alieleza.

Zuchu alisema atamtambulisha mpenzi wake hadharani kwa mara ya kwanza mnamo siku ya Valentines atakapoandalia wapendanao shoo kubwa  jijini Dar es Salaam.