Zuchu amzawadi meneja wake gari la ndoto zake

Muhtasari

•Zuchu alimtambulisha Dorice, sio tu kama meneja wake tu bali piakama  rafikiye mkubwa. 

Image: INSTAGRAM// ZUCHU

Malkia wa muziki wa Bongo Zuhura Othman almaarufu kama Zuchu alimzawadi meneja wake Dorice Mziray gari aina ya BMW alipokuwa anasherehekea siku yake ya kuzaliwa .

Zuchu alimkabidhi mwandani huyo wake wa miaka mingi zawadi hiyo ya thamani katika sherehe zilizoandaliwa nyumbani kwake jijini Dar es Salaam wikendi ambayo imetamatika.

Wakati wa sherehe hizo Zuchu alimtambulisha Dorice, sio tu kama meneja wake tu bali piakama  rafikiye mkubwa. Alimtakia maisha marefu.

"Leo ilikuwa ni sherehe ya rafiki wangu na meneja wang. Dorice  kwa wasiomjua yeye ni meneja wangu lakini pia rafiki kutoka kidato cha kwanza. Tumeng'ang'ania mpaka tukafika hapa, tuna miaka mingi tunataka tuzeeke pamoja Inshalaah. Hii ni party tulimwandalia. Sisi kama marafiki tunakupenda sana na wewe ni muhimu sana katika maisha yetu. Mimi kama rafiki wako kama tulivyozungumza tukianza safari kuwa tutawa pamoja, nina zawadi yangu ambayo nataka nikupe Inshalaah, kama itakupendeza naomba uipokee kidogo changu hiki nilichojaliwa" Zuchu alisema.

Dorice aliipokea zawadi hiyo kwa furaha na bashasha tele hadi akatiririkwa na machozi ya raha na kuishiwa na maneno.

Alisema zawadi hiyo ilimpata kwa mshangao mkubwa kwani gari alilokabidhiwa lilikuwa la ndoto zake.

"Zuchu ni rafiki wangu wa dhati wa kweli. Nina raha kubwa sana. Hili ni gari ambalo nilitaka kununua" Alisema.