Jalango aliomba msamaha, Arrow Bwoy akiri

Muhtasari

•Msanii Arrow Bwoy alieleza kuwa mtangazaji Jalango aliomba msamaha kufuatia maneno aliyotoa mwezi jana kuhusu familia yake

•Alikuwa anahojiwa na kituo kimoja cha radio nchini Kenya ambapo alieleza kuwa  Jalang’o alipita mipaka wakati alikuwa akizungumzia suala la mahusiano baina yake na Nadia Mukami

Arrow Bwoy
Arrow Bwoy
Image: instagram/AB

Msanii Arrow Bwoy alieleza kuwa mtangazaji Jalang''o aliomba msamaha kufuatia maneno aliyotoa mwezi jana kuhusu familia yake.

Arrow, ambaye alikuwa anahojiwa na kituo kimoja cha radio nchini Kenya, alieleza kuwa  Jalang'o alipita mipaka ya kuongea wakati alikuwa  akizungumza kuhusu  mahusiano baina yake na Nadia Mukami.

“Jalas ni rafiki yangu, ni mtu ambaye ameniunga mkono tangu siku ya kwanza, ni jamaa mzuri sana, bado tungali tunaongea lakini siku hio alivuka mipaka. Hakuna shida yoyote kati yetu,alinitumia ujumbe akiomba msamaha, na mimi napenda kusamehe nilimsamehe," alisema Arrow Bwoy.

Ikumbukwe Arrow Bwoy alijitokeza na kumkashifu  Jalang’o na kumuonya dhidi ya kuongea mambo yake ya familia.

Vilevile, Nadia Mukami alionyesha  ghadhabu yake kupitia  ukurusa wake wa Instagram kuhusu kitendo cha Jalang'o huku akitaja Arrow Bwoy kuwa jamaa ambaye hapendi  kuongea mambo yanayohusu familia.