'Unanifanya niwe na hisia sana,'Karen Nyamu azungumzia ujauzito wake

Muhtasari
  • Karen amekuwa mshawishi mkubwa mitandaoni, huku akitumia muda wake kutangamana na wafuasi wake mara kwa mara
Mwanasiasa Karen Nyamu Picha: RADIO JAMBO
Mwanasiasa Karen Nyamu Picha: RADIO JAMBO

Kama umekuwa mtumiaji wa mitandao ya kijamii mara kwa mara lazima uwe umekutana na Karen Nyamu wakati fulani.

Karen amekuwa mshawishi mkubwa mitandaoni, huku akitumia muda wake kutangamana na wafuasi wake mara kwa mara.

Siku kadhaa zilizopita, Karen Nyamu alifunguka kuhusu azma yake ya kisiasa ambapo atakuwa akiwania kiti cha  useneta  wa Nairobi chini ya chama cha kisiasa cha UDA.

Hili liliwaacha wengi wakijiuliza iwapo ataweza kufanya kampeni zake kwa vile ana ujauzito mkubwa wa mtoto wa pili wa mwanamuziki Samidoh.

Dakika chache zilizopita, alichapisha kwenye ukurasa wake wa instagram akizungumzia kuhusu ujauzito huo.

Kulingana naye, alisema kuwa ana nguvu na shauku ya kufanya chochote anachofanya, lakini jambo moja kuhusu ujauzito wake ni kwamba unamfanya awe na hisia nyingi.

Aliongeza na kusema hasa akiwa kanisani na wanaanza kuabudu  anaweza hata kulia.

"Ndiyo nina nguvu na shauku na ninashukuru kwa hilo! Lakini jambo moja kuhusu ujauzito wangu ni kwamba, inanifanya niwe na hisia sana😢😢 Hasa kanisani.

Pastor tu asikue fiery na worship team ikue top. Kwisha mimi hahaha asante kwa PA wangu kwa kuwa tayari na tishu," Aliandika  Karen.