Harmonize ameishiwa hela, wandani wake wanaondoka?

Muhtasari

•Baada ya habari za H-baba kusambaa  kwenye mitandao ya kijamii akiwa anamsifia mwanamuziki nguli wa Bongo Fleva, Diamond platnumz.

• Babalevo alieleza kwamba kazi aliyokuwa amepewa na bosi wake, ameifanya kwa ukamilifu kama alivyoagizwa naye

Baba Levo na Harmonize
Baba Levo na Harmonize
Image: Hisani

Baada ya habari za H-baba kusambaa  kwenye mitandao ya kijamii akiwa anamsifia mwanamuziki nguli wa Bongo Fleva, Diamond platnumz.

Mwandani wa Diamond, Babalevo kupitia ukurusa wake instagram ameandika ujumbe ambao ulionekana  kuelekezwa kwenye Kambi ya Konde Gang.

Kulingana na kauli yake, alieleza kwamba kazi aliyokuwa amepewa na bosi yake, ameifanya kwa ukamilifu kama alivyoagizwa naye.

“Bosi nimemaliza kazi,wamegundua kwamba  ukweli kwamba ‘Kilandage’ hana hela angewaua na njaa, ombi langu kwako wapokee kwa upendo kisha wape kazi wapate pesa maisha yaendelee. Ni vijana wenzetu,” aliandika Babalevo.

Kauli hii imetafsiriwa na wafuasi wa Babalevo kwamba anawakaribisha wanaohamia Wasafi kutoka KondeGang.

Ikumbukwe ni mwezi jana tu ambapo msanii Country Boy aliondoka kwenye lebo ya KondeGang, wa hivi karibuni anayekisiwa kuondoka akiwa  mwandani wa Harmonize ,H-baba.