Amber Ray amuaga Jimal Rohosafi kwaheri kwa ujumbe wa kihisia na kufuta tattoo ya jina lake

Muhtasari

•Ili kuthibitisha kuwa hataki tena kuhusishwa na mfanyabiashara huyo, Amber Ray sasa amefuta tatoo ya jina lake ambayo  alikuwa amechorwa mgongoni.

•Wakati mapenzi yao yalikuwa yamenoga, mwanasoshalaiti huyo alichukua hatua kubwa ya kuchorwa jina la kati la milionea huyo 'Marlow'

Amber Ray na Jimal Rohosafi
Amber Ray na Jimal Rohosafi
Image: INSTAGRAM

Hatimaye mwanasoshalaiti Faith Makau almaarufu kama Amber Ray amethibitisha kuwa tayari  amesonga mbele na maisha yake na hayuko tayari kurudiana na aliyekuwa mpenzi wake Jimal Marlow  Rohosafi.

Ili kuthibitisha kuwa hataki tena kuhusishwa na mfanyabiashara huyo, Amber Ray sasa amefuta tatoo ya jina lake ambayo  alikuwa amechorwa mgongoni.

Amber Ray alifahamisha wafuasi wake kuhusu hatua hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambako alipakia video inayoonyesha jinsi ilivyofanyika.

Mama huyo wa mtoto mmoja aliambatanisha video hiyo na ujumbe wa kumpungia mpenzi huyo wake wa zamani kwaheri.

"Kwa kweli sijuti mapenzi  niliyokupa kwa sababu labda uliyahitaji" Amber Ray alisema.

Amber Ray pia alimtumia Jimal ujumbe mwingine wa kwaheri katika wimbo wa reggea 'Last Time'  wake Sharieta.

Mwaka jana wawili hao walikuwa kwenye mahusiano ya kuja na kwenda kwa kipindi cha miezi kadhaa.

Wakati mapenzi yao yalikuwa yamenoga, mwanasoshalaiti huyo alichukua hatua kubwa ya kuchorwa jina la kati la milionea huyo 'Marlow'

Mahusiano yao yalikabiliwa na drama sio haba na hata kusababisha ndo ya kwanza ya Jimal kusambaratika.

Mke wa kwanza wa mwenyekiti huyo wa baraza la wamiliki matatu jijini Nairobi, Amira aliomba talaka baada ya kuchoshwa na vituko vilivyoingilia ndoa yao.