Naiogopa siku ambayo binti yangu ataniuliza kuhusu kilichotokea- Ex wa Mulamwah akiri

Muhtasari

•Muthoni alisema aliweka wazi kuwa anajivunia bintiye Keilah Oyando na anafurahia sana kumlea.

•Alikiri kwamba hajajiandaa kwa siku ambayo binti yake atamuliza kuhusu drama zote zilizotokea katika kipindi cha kuzaliwa kwake.

Image: INSTAGRAM// CAROL SONNIE

Mwigizaji Caroline Muthoni amedhihirisha kuwa mtoto wake angali anaendelea vyema licha yake kutengana na mzazi mwenzake David Oyando almaarufu kama Mulamwah miezi kadhaa kabla ya kujifungua.

Akiwa kwenye mahojiano na Eve Mungai, Muthoni alisema aliweka wazi kuwa anajivunia bintiye Keilah Oyando na anafurahia sana kumlea.

"Mtoto Keilah ako sawa, amenenepa sana. Anaendelea vizuri na nafurahia. Namshukuru Mungu sana" Muthoni alisema.

Muthoni alipuuzilia mbali uvumi kuwa mahusiano yake na Mulamwah yaligonga ukuta kutokana na utata kuhusu baba mzazi wa mtoto wake huku akidhihirisha bayana kuwa bintiye aliiga sura ya mchekeshaji huyo.

Mwigizaji huyo alikiri kwamba hajajiandaa kwa siku ambayo binti yake atamuliza kuhusu drama zote zilizotokea katika kipindi cha kuzaliwa kwake.

"Kusema ukweli sijui nitamwambia nini. Naogopa. Akiniuliza swali hilo sijui nitamwambia  nini. Natumai ataelewa lakini" Muthoni alisema.

Muthoni na Mulamwah walitangaza kutengana kwao mnamo mwezi Oktoba mwaka jana, miezi michache tu baada ya kuzaliwa kwa binti yao.

Wapenzi  hao wa zamani walifichua kwamba waliafikia uamuzi wa kutengana hata kabla ya Keilah kuzaliwa.