"Sijui nilifanya nini ili nistahili wewe" Diana B amsherehekea mumewe Bahati kwa kumpa zawadi ya gari

Muhtasari

•Mwanamuziki huyo alimkabidhi mkewe gari aina ya Prado Toyota TX kama zawadi ya tatu ya Valentines.

•Hapo awali Bahati alitangaza kwamba atakuwa anamkabidhi mkewe zawadi tatu katika msimu huu wa wapendanao.

Image: INSTAGRAM//DIANA MARUA

Wanandoa maarufu Kelvin Bahati na Diana Marua wameendelea kutoa changamoto kubwa kwa wanandoa wengine kuhusu jinsi ya kusherehekea penzi lao.

Siku chache tu baada ya Bahati kumnunulia mama huyo wa watoto wake kipande cha shamba kama zawadi ya Valentines, mwanamuziki huyo sasa amesurprise kipenzi chake na zawadi nyingine kubwa ya gari.

Mwanamuziki huyo alimkabidhi mkewe gari aina ya Prado Toyota TX kama zawadi ya tatu ya Valentines.

"Zawadi ndogo tuya Valentines kwa mke wangu. Furahia zawadi yako ya tatu mpenzi wangu Diana Marua" Bahati alisema.

Diana Marua ambaye hivi majuzi alijitosa kwenye tasnia ya muziki akijitambulisha kama rapa Diana B alizamia kwenye mtandao wa Instagram kusherehekea zawadi hiyo huku akimshukuru mumewe kwa kumtimizia ndoto zake.

"Sina neno, sina la kusema, Sipumui. Asante mpenzi  Bahati. Tumetoka mbali na tunaweza kufika mbali zaidi kutoka hapa. Umetimiza ndoto zangu zote. Gari hili ni zawadi yangu kwa bidii yangu katika kutengeneza content, bado nimeshtuka. Shukran. Sijui nilifanya nini ili nistahili wewe. Kila siku, namshukuru Mungu kwa ajili yako. Daima akupe neema kati ya wanaume wengine. Nakupenda Bahati" Diana alisema.

Rapa huyo chipukizi alitangaza kwamba gari hilo limeandikishwa kwa jina lake kuashiria kwamba yeye ndiye mmiliki rasmi.

Hapo awali Bahati alitangaza kwamba atakuwa anamkabidhi mkewe zawadi tatu katika msimu huu wa wapendanao.