Madai kuwa Lilian Ng'ang'a na Juliani wanatarajia mtoto wao wa kwanza yaibuka

Muhtasari

•Madai haya yametibuka baada ya Lilian kuchapisha video inayoonyesha tumbo lake likiwa limechoza, ishara tosha kuwa huenda ni mjamzito.

•Pete ambayo Lilian alivishwa na kipenzi chake Juliani  siku ya harusi yao  inaonekana vizuri katika video ambayo alichapisha.

Juliani na mke wake Lilian Nganga
Juliani na mke wake Lilian Nganga
Image: HISANI

Mambo yanaonekana kuendelea kuwaendea vyema wanandoa wapya Lilian Ng'ang'a na Juliani huku sasa madai yakiibuka kuwa wanatarajia tunda la kwanza la mahusiano yao, mtoto.

Madai haya yametibuka baada ya Lilian kuchapisha video inayoonyesha tumbo lake likiwa limechoza, ishara tosha kuwa huenda ni mjamzito.

Katika video hiyo mchumba huyo wa zamani wa gavana Alfred Mutua alionekana akijivinjari ufukweni huku akionekana mwenye bashasha tele.

"Siku ya wapendanao 2022" Lilian aliandika chini ya video hiyo.

Haya yanajiri wiki chache tu baada ya wanandoa hao kufunga pingu za maisha katika hafla ndogo iliyohudhuriwa na familia na marafiki wa karibu kwenye kiwanja cha Paradise Garden.

Pete ambayo Lilian alivishwa na kipenzi chake Juliani  siku ya harusi yao  inaonekana vizuri katika video ambayo alichapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram siku ya Valentine's.

Wanandoa hao wawili walikuwa katika eneo la Pwani wikendi iliyopita ambako Juliani alikuwa anatumbuiza katika tamasha ya 'Beats and Eat'

Habari za ujauzit zinakuja miezi michache tu baada ya mahusiano yao kujulikana wazi kufuatia kukatizika kwa mahusiano ya Lilian na gavana Mutua.