Lucy Natasha akana madai ya kutoa miujiza ya uongo

Muhtasari

• Mhubiri Lucy  Natasha amefunguka kuhusu uvumi uliokuwa ukienezwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba huwa anafanya miujiza ya uongo.

• Natasha na Mume wake mwenye asili ya Kihindi walisema watu wanaowachukia hutunga hadithi za uongo ili kufanya ionekane kama wao ni  waongo na  wanafanya miujiza ya isiyo ya kweli.

 

Mhubiri Lucy Natasha na mpenzi wake Prophet Carmel
Mhubiri Lucy Natasha na mpenzi wake Prophet Carmel
Image: FACEBOOK// LUCY NATASHA

Mhubiri Lucy  Natasha amefunguka kuhusu uvumi uliokuwa ukienezwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba huwa anafanya miujiza ya uongo.

Natasha na Mume wake mwenye walisema watu wanaowachukia hutunga hadithi za uongo ili kufanya ionekane kama wao ni  waongo na  wanafanya miujiza ya isiyo ya kweli.

Kupitia mahojiano na Lynn Ngugi kwenye chaneli yake ya Youtube walisema waumini wake  hawapaswi kuamini wanachokisema wanamitaandao kwani matendo yao yanaonyesha kuwa wanafanya miujiza ya ukweli na washirika wanatoa ushuhuda kuhusu miujiza yao.

"Watu wanachagua vitu na kutunga hadithi   bila kufikiria wanachotaka kusema, tunawaita watu madhabahuni kwa sababu tofauti kwa sababu nilikuombea wiki iliyopita haimaanishi kuwa sitakuombea tena wiki inayofuata," alisema mhubiri Natasha.

Aliongeza kuwa kanisa ni kama hospitali ambapo unaweza tembea wakati wowote unaohitaji  matibabu ya aina zote.

 "Kanisa ni kama hospitali kwa hivyo unaomba kwa ajili ya watu tofauti kwa masuala tofauti. Mtu yule yule anaweza kuwa anahitaji uponyaji au ndoa, kwa hiyo haya ni madai ya uwongo."