'Nilipachikwa mimba kisha nikatemwa' Kanambo asema

Muhtasari

•Kanambo Quincher ameeleza changamoto alizokumbana nazo wakati alikuwa anaibukia kwenye tasnia ya muziki

•Kanambo alisimulia maisha yake yalibadilika wakati alipata ujauzito akiwa na umri wa miaka 17.

 

 

Kanambo Quincher na King Kaka
Image: Instagram

Mwanamuziki chipukizi  Kanambo Quincher ameeleza changamoto alizokumbana nazo wakati alikuwa anaibukia kwenye tasnia ya muziki.

Kulingana naye alipachikwa mimba wakati alikuwa angali mwanafunzi wa shule ya upili.

Kanambo alisimulia kuwa maisha yake yalibadilika wakati alipata ujauzito akiwa na umri wa miaka 17.

“mimi ni mzaliwa wa kwanza katika familia ya wasichana wawili, haikuwa rahisi kupata ujauzito lakini muda uliponiponya. Siwezi kumshauri msichana yeyote kutoa mimba, leo naweza kusema kwa fahari mimi ni mama,” alisema Kanambo.

Kanambo alisajiliwa na lebo ya King Kaka ambayo ilimsimamia kutoa kibao cha kwanza ambacho kinajulikana ‘Walai’

Alieleza kuwa mamake amekuwa mshauri mkubwa na  kueleza kuwaomba wasichana kuwa kuavya mimba sio  kitu kizuri.