Simjui! Shoga Silas Miami amemkana babake Louis Otieno hadharani

Muhtasari

• Silas Miami ni mtengeneza filamu ambaye anajulikana na wengi kama shoga hasa baada ya kuweka bayana mitandaoni kwamba ana mahusiano na mwanaume mzungu.

• Miami alisema kwamba babake ndiye alimkataa mwanzo na kisha kutaka uswahiba na yeye baada ya kugundua kwamba anaweza akatengeza pesa kutoka kwake.

Silas Miami na babake Louis Otieno
Image: Mpasho

Silas Miami ni mtengeneza filamu ambaye anajulikana na wengi kama shoga hasa baada ya kuweka bayana mitandaoni kwamba ana mahusiano na mwanaume mzungu. Ni mwanawe mtangazaji mkongwe Louis Otieno na kijana huyo amesema kwamba wengi wanamjua kama mwanawe Otieno lakini yeye hamjui na kusema kwamba angekutana na babake huyo kwa mara tatu tu, lakini safari za kwanza mbili zilitibuka na mara ya kwanza kukutana uso kwa uso ikiwa ni wakati ako na umri wa miaka 22.

Miami ambaye anaishi nchini Afrika Kusini na mpenzi wake mzungu akionekana kujibu swali lililoibuliwa na mwanahabari wa NTV James Smart, alisema kwamba nusra wakutane na babake huyo ambaye pia ni mtangazaji mkongwe wa runinga ya KTN wakati akiwa na umri wa miaka minne lakini haikutokea.

“Sikuwa naongeza chumvi maneno yangu wakati nilisema kwamba ningekutana na Louis mara tatu katika maisha yangu yote. Inafaa ijulikane kwamba mara ya kwanza nimekutana na yeye ni wakati nilikuwa na miaka 22,” aliandika Silas

Katika ujumbe mrefu ambao mtengeneza filamu huyo aliachia kwenye ukurasa wake wa Twitter, alisema kwamba anajua kwamba Louis ni babake wad amu lakini hamjui wala hamtambui.

“Kusema kweli, kwa miaka mingi, watu wachache sana ndio walikuwa wakijua kwamba huyo ni babangu. Louis aliweka wazi kwamba hakutaka kuhusishwa na chochote na mimi. Niliteseka sana na tamko hilo, iliniuma sana kwa njia nyingi zisizoweza kufikirika,” aliandika Miami.

Alieleza kwamba katika tukio hilo la kukutana na babake akiwa na miaka 22, Miami alisema kwamba alipokea habari kuwa babake ni mgonjwa sana na hapo ndipo aliabiri ndege kuja Nairobi na kwa mara ya kwanza akakutana na yeye na Louis amkataa na kumkana kwamba si mtoto wake.

“Nilipofika kitandani pake, alitumia dakika za kwanza mbili kunikana kama mtoto wake mpaka pale alipogundua kwamba anaweza tengeneza pesa kutoka kwangu. Hapo ndipo niligundua kwamba nimekuwa nikitumia muda mwingi tu kujiumiza akili na mawazo kwa mtu ambaye hakuwa tayari hata kunitambua,” aliandika Miami.

Ila alisisitiza kwamba lengo lake kuu si kumdhalilisha mwanahabari huyo mkonge bali ni kuwekwa wazi ukweli wa mambo na kuwataka watu wakome kumuulizia kuhusu mtu ambaye hamjui.

“Huyu mwanaume hanijui. Na mimi simjui vilevile,” aliamliza Miami.