Aliniambia atabadilisha mtoto jina na amwambie babake alikufa- Mulamwah alalamika kuhusu EX

Muhtasari

•Mchekeshaji huyo amefichua kuwa Muthoni aliapa kubadilisha jina la binti yao na kumdanganya kuhusu aliko babake wakati atakapouliza.

•Aliendelea kufichua kuwa Muthoni alikataa kabisa kumhusisha yeye na familia yake katika maisha ya mtoto wao.

Image: INSTAGRAM// MULAMWAH

Mchekeshaji mashuhuri David Oyando amefunguka zaidi kuhusu mvutano uliopo kati yake na aliyekuwa mpenziwe Carrol Sonnie kuhusiana na suala la mtoto wao.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mulamwah amesema mpenzi huyo wake wa zamani  ameweka vikwazo vingi kati yake na binti yao wa miezi mitano na hafahamu mengi kuhusu maendeleo yake.

Mchekeshaji huyo amefichua kuwa Muthoni aliapa kubadilisha jina la binti yao na kumdanganya kuhusu aliko babake wakati atakapouliza.

"Kusema kweli hata sijui kama bado anaitwa Keilah. Mama yake aliniambia kuwa atabadili majina yake na amwambie kuwa babake alikufa" Mulamwah alijibu shabiki aliyetaka kufahamu iwapo huwa anapata nafasi ya kuona bintiye.

Aliendelea kufichua kuwa baada ya kutengana Muthoni alikataa kumhusisha yeye na familia yake katika maisha ya mtoto wao.

"Familia yangu hata haijawahi kuona mtoto huyo, alikataa kumleta nyumbani. Hata alimnyoa mwenyewe kinyume na tamaduni" Mulamwah amefichua.

Muthoni kwa upande wake ameapa kusalia kimya kuhusiana na madai ya mpenzi huyo wake wa zamani kutokana na heshima yake kwa bintiye.

"Kwa heshima niliyo nayo kwa Keila, bado nachagua kusalia kimya" Muthoni amejibu kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Mulamwah na Muthoni walitangaza kutengana kwao mnamo mwezi Desemba mwaka jana, miezi mitatu tu baada ya Keilah kuzaliwa.

Wawili hao walifichua kuwa walitengana miezi mingi kabla ya binti yao kuzaliwa wakati ujauzito wa Muthoni ulikuwa na miezi mitatu tu.