Mulamwah adai mpenziwe alijaribu kuavya mimba ya miezi 3

Muhtasari

•Mulamwah amedai kwamba alitia juhudi kubwa  kuhifadhi ujauzito huo baada ya kugundua kuwa mpenzi huyo wake wa zamani alikuwa anameza tembe za kuuavya.

•Pia amemkashifu mpenzi huyo wake wa zamani kwa kuwa na mahusiano na jamaa mwingine ambaye walishirikiana naye kupanga uzazi.

•Carrol Sonnie kwa upande wake amesema anachagua kusalia kimya licha ya yote yanayosemwa dhidi yake.

Image: INSTAGRAM// MULAMWAH

Mcheshi David Oyando almaarufu kama Mulamwah amedai kwamba aliyekuwa mpenzi wake Carrol Sonnie alijaribu kuavya mimba ya bintiye alipokuwa mimba ya miezi mitatu tu. 

Kupitia video ambayo ameweka kwenye ukurasa wake wa Instagram, Mulamwah amedai kwamba alifanya juu chini kutunza ujauzito huo baada ya kugundua kuwa mpenzi alikuwa anameza tembe za kuuavya.

Mulamwah amedokeza kuwa suala hilo ndilo lilichangia kutengana kwao takriban miezi sita kabla ya mtoto kuzaliwa.

"Huyo mtoto mnaona akibebwa na kupigwa picha saa hizi, mnajua mamake alikuwa amemtoa kweli? Akiwa na ujauzito wa miezi mitatu alikuwa ashameza tembe, mtoto alikuwa anatoka. Mimi niligundua kuchelewa kuwa alikuwa anafanya hivo. Nilienda hospitali nikatumia pesa sijui ngapi kuhifadhi ujauzito huo" Mulamwah amedai.

Pia amemkashifu mpenzi huyo wake wa zamani kwa kuwa na mahusiano na jamaa mwingine ambaye walishirikiana naye kupanga uzazi. Amedai kuwa Sonnie hata hakuwa na uhakika kuhusu baba halisi wa mtoto ambaye alikuwa amebeba.

Mchekeshaji huyo amesema kuwa amelazimika kuvunja kimya kuhusu yaliyotokea baada kuona mzazi mwenzake bado analizungumzia suala hilo.

"Msidhani mambo yanatendeka hivo tu. Kuna sababu za kila kitu. Tukiamua kuongea maisha ya watu itaharibika huku nje. Stori ni mingi. Mambo yanaharibika. Tunajaribu kunyamaza na kutoa watu mitandaoni na hawasikii" Amesema.

Carrol Sonnie kwa upande wake amesema anachagua kusalia kimya licha ya yote yanayosemwa dhidi yake.

"Kwa heshima niliyo nayo kwa Keila na kwangu mwenyewe, , bado nachagua kusalia kimya" Sonnie alisema kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Mwigizaji huyo pia aliambia Mpasho :"Niko makini sana juu ya nini cha kuzungumza mbele ya watu. Binti yangu anakua na atasoma mambo haya yote."