Sitaki kuwa baba!, asema mjukuu wa Mwai Kibaki

Muhtasari

Mjukuu wa aliyekuwa rais wa tatu wa Kenya Mwai Kibaki amesema kwamba yeye hana mpango wowote wa kuwa baba na kamwe hawazii suala la kuwa na watoto.

Sean Andr3w
Image: Instagram

Mjukuu wa aliyekuwa rais wa tatu wa Kenya Mwai Kibaki amesema kwamba yeye hana mpango wowote wa kuwa baba na kamwe hawazii suala la kuwa na watoto.

Sean Andrew, 25, ambaye ni mwanamitindo wa kibiashara amejibu swali la mtu aliyemuuliza kwenye Instagram yake kuhusu kuwa na watoto na akasema amekuwa akijua tangu kitambo kwamba hataki kuwa baba.

“Mbona hutaki kuwa baba siku moja?” mmoja kati ya mashabiki wake aliuliza.

“Ni vile tu sitaki watoto. Hicho ni kitu nimekuwa nikijua kwa muda sasa,” alijibu Andrew.

Image: INSTAGRAM

Hii si mara ya kwanza anasema hivyo kwani mwaka jana alipoulizwa swali kama hilo pia alikataa na kusema hataki kuwa baba.

Wakati huo aliulizwa iwapo amewahi fikiria siku moja kuoa na kutulia katika ndoa na kuwa na watoto.

“Ndio nimewahi fikiria kuoa na kutulia katika ndoa lakini hata siku moja sijawahi jifikiria au kujiona kuwa baba. Pengine niwe mume tu lakini sitaki watoto,” alijibu Andrew.

Mwanamitindo huyo alizungumzia maamuzi yake hayo na kusema kwamba yalitokana na yeye kujiona hana bahati katika mapenzi kwani amewahi kuwa katika mahusiano Zaidi ya moja lakini akaishia kuvunjwa moyo.