Meneja wa Harmonize amtetea Diamond kuhusu video ya Gidi

Muhtasari

•Choppa ameeleza kuwa Diamond anaweza kuwa alitumia bendera hiyo kimakosa  na inapaswa watu waelewe.

•Bendera hio ambayo ilitumiwa sana na Marekani kama ishara ya ubaguzi dhidi ya Wamerika  wenye asili ya Kiafrika

 

Diamond Platnumz
Diamond Platnumz
Image: HISANI

Meneja wa Harmonize, Choppa amefunguku kuhusu video ya mwanamuziki mashuhuru Diamond Platnumz, Gidi ambayo imekuwa ikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii kwa kutumia bendera ya muungano wa marekani.

Bendera hio ambayo ilitumiwa sana na Marekani kama ishara ya ubaguzi dhidi ya Wamerika  wenye asili ya Kiafrika.

Kupitia kituo kimoja cha habari nchini humo, Choppa ameeleza kuwa Diamond anaweza kuwa alitumia bendera hiyo kimakosa inapaswa watu waelewe na kumsamehe kwa sababu ni kitu ambacho hakijawai tokea kwenye video zake za hapo awali.

 

"mimi nafikiri kabla ya watu kulaumu au kuendelea kuvikuza hivi vitu ambavyo ni vidogo wakati mwingine ni vidogo lakini vinakuzwa vinakuwa vitu vikubwa sio kitu sahihi uenda alifanya kwa nkutokujua au halijisahau sidhani kama yeye anaweza akawepa kitu ambacho kitawaumiza watu weusi hilo kikweli sidhani kama linaweza hilo," alisema Choppa.