Presha zimezidi! Hatimaye Fash Hussein asema atarudishia DJ Shiti mtoto

Muhtasari

• Aliyekuwa mke wa mchekeshaji DJ Shiti, Fash Hussein hatimaye ametagangaza kwamba atamrudisha mtoto kwa baba yake siku chache baada ya wawili hao kutofautiana mitandaoni kuhusu malezi ya mwanao.

dj-shiti-2
dj-shiti-2

Aliyekuwa mke wa mchekeshaji DJ Shiti, Fash Hussein hatimaye ametagangaza kwamba atamrudisha mtoto kwa baba yake kwa sababu amepata unyongovu na msongo wa mawazo.

Hussein ameandika kwenye instastories zake akisema kwamba sasa ndio anaamini unyongovu na msongo wa mawazo ni jambo la kweli na kusema kwamba hata siku moja hakuwahi fikiria kumrudisha mwanao Miriam kwa baba yake ambaye ni DJ Shiti lakini kwa sababu amebanwa Zaidi ya maelezo basi hana jinsi ila  kurudisha mtoto kwa babake.

“Sikuwahi kabisa kuwa na dhamira la kuchoka na binti yangu kwa njia yoyote ile, lakini kwa kile ambacho nimekuwa nikikipitia, nimeamua kumrudisha mtoto kwa babake. Huu ni uamuzi mgumu kuufanya lakini ni wa maana,” aliandika Hussein.

Vile vile Fash Hussein amesema kwamba anatamani mwanawe atakua kwa haraka na mapenzi makubwa na akuje kugundua kwamba uamuzi wa mamake kumrudisha kwa babake mzazi si kumtupa bali ni kutokana na mapenzi ya dhati.

“Ninatumai binti yangu atakua na kuwa binadamu wa ajabu kabisa na naomba daima akae akijua kwamba maamuzi haya ni kutokana na mapenzi yangu kwake,” aliandika Fash katika ujumbe huo wenye uchungu.

Maamuzi haya yanakuja siku chache tu baada ya wawili hao kupakana matope mitandaoni huku Fash akimshtumu Shiti kwamba hatoi hela ya kukidhi mahitaji ya mwanao na kusema kwamba mchekeshaji huyo huto shilingi 150 za Kenya pekee, ambapo Shiti alimjibu kwa kutoa wimbo wa kukejeli matamshi hayo ya Fash kwamba anashughulikia mtoto kwa shilingi 150 pekee.

Image: ISTAGRAM

Je, unahisi maamuzi ya Fash kurudisha mtoto kwa babake ni ya kweli na haki kwa mtoto ama ameboronga?