Hongera! Karen Nyamu ajifungua mtoto wa kike

Muhtasari

•Inaaminika kuwa Samidoh ndiye baba ya mtoto huyo wa tatu ingawa wawili hao hawajakuwa  katika hali ya kuelewana kwa muda mrefu.

•Mapema wiki hii mwanasiasa huyo alifichua kuwa anatajia mtoto wa kike na kudokeza kuwa bintiye ataitwa Njeri.

Image: INSTAGRAM// KAREN NYAMU

Wakili na mwanasiasa Karen Nyamu amejifungua mtoto wa tatu

Nyamu ambaye anawania kiti cha useneta katika uchaguzi wa mwezi Agosti ametangaza habari za kubarikiwa na mtoto wa kike  kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Mwanasiasa huyo asiyepungukiwa na utata amepakia picha maridadi ya mikono ya mtoto na kuiambatanisha na ujumbe, "Tunakupa utukufu wote. Tunakuabudu wewe Mungu wetu."

Image: INSTAGRAM// KAREN NYAMU

Kifungua mimba wa nyamu ni binti ambaye alipata na mpenzi wake wa zamani DJ Kelvin huku wa pili akiwa mvulana ambaye alipata na nyota wa mugithi Samuel Muchoki almaarufu Samidoh.

Inaaminika kuwa Samidoh bado ndiye baba ya mtoto huyo wa tatu ingawa wawili hao hawajakuwa  katika hali ya kuelewana kwa muda mrefu.

Hivi majuzi Nyamu alizua mdahalo mitandaoni baada ya kuchapisha ujumbe ulioashiria kuwa huenda Samidoh sio baba mzazi wa mtoto huyo kama inavyoaminika na wengi.

“Aache kujishuku, hajaambiwa mimba ni yake” Nyamu alijibu shabiki aliyetaka kujua iwapo mwanamuziki huyo alikubali ndiye mhusika katika ujauzito hou.

Mapema wiki hii mwanasiasa huyo alifichua kuwa anatajia mtoto wa kike na kudokeza kuwa bintiye ataitwa Njeri.