Amber Ray atambulisha kipenzi kipya miezi baada ya kutengana na Jamal Roho Safi

Muhtasari

•Wawili hao walidokeza mahusiano yao kupitia mtandao wa Instagram ambako walipakiana na kuandika jumbe zilizoashiria mapenzi.

•Haya yanajiri wiki chache tu baada ya Amber Ray kumuaga kwaheri aliyekuwa mpenziwe Jimal Rohosafi na kufuta tattoo ya jina lake ambayo alikuwa amechorwa mgongoni.

Image: INSTAGRAM// AMBER RAY

Miezi kadhaa baada ya kutengana na mfanyibiashara Jamal Marlow Rohosafi, mwanasoshalaiti mashuhuri Faith Makau almaarufu Amber Ray anafahamika kujinyakulia kipenzi kipya.

Mama huyo wa mtoto mmoja anaaminika kuwa kwenye mahusiano na mchezaji mipira ya vikapu IB Kabba kutoka Sierra Leone.

Wawili hao walidokeza mahusiano yao kupitia mtandao wa Instagram ambako walipakiana na kuandika jumbe zilizoashiria mapenzi.

Amber Ray alichapisha picha yake na Kabba wakila chakula pamoja katika mgahawa wa kifahari na kuiambatanisha na ujumbe "Picha ninayoipenda zaidi 🥰🤗" 

Kabba alipakia picha hiyo hiyo kwenye ukurasa wake wa Instagram na kudai kuwa ndiyo aipendayo zaidi.

Image: INSTAGRAM// AMBER RAY

Isitoshe mchezaji huyo wa kimataifa wa mpira wa kikapu pia alipakia picha nyingine ya Amber Ray na kumtambulisha mwanasoshalaiti huyo kama mpenzi wake.

Haya yanajiri wiki chache tu baada ya Amber Ray kumuaga kwaheri aliyekuwa mpenziwe Jamal Rohosafi na kufuta tattoo ya jina lake ambayo alikuwa amechorwa mgongoni.

Mwaka jana wawili hao walikuwa kwenye ndoa isiyo imara ambayo ilisheheniwa na drama kochokocho.

Ndoa hiyo ya miezi michache ilisababisha kusambaratika kwa ndoa ya kwanza ya Jamal na mama ya watoto wake wawili Amira.