Esther Musila ajibu kuhusu kupata watoto na Guardian Angel

Muhtasari
  • Shabiki mmoja alimuuliza Esther kama amefikiria kupata mtoto na Guardian Angel
Image: INSTAGRAM// GUARDIAN ANGEL

Uhusiano na ndoa yake Esther Muslia na msanii wa nyimbo za injili Guardian Angel haukupokelewa vyema na baadhi ya wanamitandao.

Wapenzi hao wawili walikejeliwa mitandaoni, ilhali hawakuzingatia maoni hasi ya mashabiki.

Baada ya wawili hao kufunga pingu za maisha wanamitandao na mashabiki wamekuwa wakiuliza kama wawili hao watapata mtoto au watoto pamoja.

Kwa wale wote wanaouliza ni lini atapata mtoto na Guardian, Esther huwa anawajibu kwamba wanapaswa kuzingatia maisha yao.

Kupitia kwenye mitandao ya kijamii ya instagram sekta ya Q &A swali kama hilo liliibuka.

Shabiki mmoja alimuuliza Esther kama amefikiria kupata mtoto na Guardian Angel.

Alijibu; "Sina budi kufikiria."

Wengine walimsifu Esther kwa kumfanya Angel Guardian kukua kiroho na kiakili.

"Guardian siku zote amekuwa mtu wake mwenyewe na mwenye umakini mkubwa. Nina furaha kuwa mimi ni sehemu ya safari yake maishani," alisema.

Kuhusu maoni mabaya yanayohusu uhusiano wao, Esther alisema;

"Siwaburudishi kwa urahisi,Sitawahi kuishi maisha ya mtu yeyote ila yangu."

Pia alifichua kwamba mwaka huu msanii huyo atatoa albamu.