Hongera Baba Njeri! Wanamitandao wampongeza Samidoh baada ya Karen Nyamu kujifungua

Muhtasari

•Mtoto aliyezaliwa Jumamosi ni wa tatu wa Nyamu na inaaminika kuwa ni wake wa pili na mwanamuziki Samidoh.

•Mamia ya wanamitandao wamekita kambi kwenye kurasa za Samidoh za mitandao ya kijamii kumpongeza kwa mtoto ambaye hajathibitisha mwenyewe kuwa ni wake.

Samidoh na Karen Nyamu
Samidoh na Karen Nyamu
Image: INSTAGRAM

Staa wa Mugithi Samuel Muchoki almaarufu kama Samidoh amekuwa akipokea jumbe kochokocho za pongezi siku za hivi majuzi.

Jumbe hizo zilianza kufurika kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii siku ya Jumamosi baada ya wakili na mwanasiasa Karen Nyamu kutangaza habari za kujifungua  mtoto wa kike.

 Nyamu alipakia picha maridadi ya mikono ya mtoto na kuiambatanisha na ujumbe, "Tunakupa utukufu wote. Tunakuabudu wewe Mungu wetu."

Mtoto aliyezaliwa Jumamosi ni wa tatu wa Nyamu na inaaminika kuwa ni wake wa pili na mwanamuziki Samidoh.

Mwanasiasa huyo aliyezingirwa na utata mwingi tayari ana mtoto mwingine wa mwaka mmoja na Samidoh. Licha ya wawili hao kuwa wazazi wenza, uhusiano wao hata hivyo umekabiliwa na changamoto tele katika siku za hivi karibuni.

Miezi michache iliyopita Bi Nyamu alimshtumu Samidoh kwa kumshambulia na kumvunjia simu yake. Wakati huo mgombeaji  huyo wa useneta wa Nairobi alifichua kuwa Samidoh ndiye baba ya mtoto ambaye alikuwa amebeba.

Kutokana na hayo wanamitandao bado wanaamini kuwa mwanamuziki huyo ndiye baba mzazi  wa mtoto wa Bi. Nyamu. Mamia ya wanamitandao wamekita kambi kwenye kurasa za Samidoh za mitandao ya kijamii kumpongeza kwa mtoto ambaye hajathibitisha mwenyewe kuwa ni wake.

Hizi baadhi ya jumbe za watumizi wa Instagram;-

@graciouse_success Hongera Baba Njeri Muchoki. Ulifanya kazi nzuri

@kiksjulie Wewe sasa ni baba wa watoto watano. Hongera

@supuu_nice Sawa amePUSH na hivi wewe ndiye baba mpya mtaani

@janicenjoka Hongera kwa mtoto wa kike

@Sarah_kangogo Ushamtembelea Njeri?