Rayvanny na Harmonize wajibandika majina ya matajiri baada ya Diamond

Muhtasari

• Alianza Diamond kwa kujiita Dangote, sasa Harmonize amefuata kwa kujiita Bakhresa naye Rayvanny hakuachwa nyuma kwani amejiita Bill Gate.

Harmonize, Rayvanny
Image: Maktaba

Wasanii wa bongo flevqa wanaendelea kuwac na ndoto nzuri za utajiri katika kazi zao za muziki. Wasanii wengi tu wamekuwa kwa muda mrefu wakizifuata nyayo za matajiri tajika duniani na hata kujibandika majina yao kama majazi.

Ilianza na msanii Diamond Platnumz kujipa jina la kimajazi la Dangote, ambaye ni bilionea Tajiri nambari moja katika bara la Afrika kulingana na orodha ya Forbes. Diamond alijiita jina hilo ambalo limezoeleka na wengi mpaka wengine kulivusha mipaka hadi kwa familia yake ambapo wanamwita mama yake kuwa ‘Mama Dangote’

Bila shaka maana ya msanii huyo kulikumbatia jina la Tajiri huyo mfanyibiashara ni kutokana na kupendezwa au tuseme kuhimizwa na utajiri wake, wengi wakihoji kwamba ni kujivika kilemba hicho ili kuwa katika mkondo sawa wa kufuata mfano wake katika kupata utajiri wake kimuziki na kibiashara pia ambapo tangia hapo Diamond amekuwa ni mfanyibiashara mkubwa nchini Tanzania akianzisha shirika la habari la Wasafi na hivi karibuni alizundua kampuni ya ubashiri almaarufu Wasafi Bet.

Harmonize na Rayvanny nao hawajaachwa nyuma kwani wamekuwa wa hivi punde kukumbatia majina ya matajiri wakubwa duniani ambao wanawaita kama ‘role models’ wao katika kuukimbizia utajiri.

Harmonize wiki iliyojipa alianza kujiita jina la Bakhresa, ambalo ni jina la Said Salim Bakhresa ambaye ni mfanyibiashara Tajiri katika nchi ya Tanzania na Afrika Mashariki mwenye kampuni nyingi chini ya mwavuli wa Bakhresa. Akitangaza tamasha lake ambalo alikuwa analipanga katika mji wa Mwanza, Harmonize alikuwa anajiita Bakhresa na kuwaambia mashabiki wake kwamba ‘Bakhresa yuko njiani’.

Image: Instagram

Inaonekana hili pia lilimfikia msanii Rayvanny ambaye siku ya jana amepakia video yenye umati mkubwa wa wafuasi na mashabiki wake wakimpokea na kusema kwamba anafaa aitwe Bill Gate kutokana na utajiri mkubwa wa ushabiki alionao. Bill Gate ni Tajiri namba tatu kote duniani na msanii huyo amelikumbatia jina hili akipania kulenga utajiri mkubwa pia katika ndoto zake. Rayvanny mpaka ametoa kibao kwqa jina hilo na kusema kwamba mtu yeyote anazidi kupambana kutafuta hela kama yeye basi ni Bill Gate kivyake.

Instagram

Je, wewe unahisi msanii unayemfuatilia kwa ukaribu anafaa ajiite jina gani la majazi?