Zari akiri kumpenda Diamond hata zaidi," Kuliko tulivyokuwa kwenye ndoa"

Muhtasari

•Zari akizingumza kuhusu mahusiano yake mapya na GK Choppa alieleza kuwa amekuwa akijaribu kumchumbia kwa takriban miaka mitatu.

•Alifafanunua kuhusu uhusiano wake na Diamond Platnumz na kudai kuwa hawajawahi kurudiana ila wana ukaribu mkubwa ikizingatiwa kwa kuwa wao ni wazazi wenza.

Zari The Boss Lady
Zari The Boss Lady
Image: Hisani

Mwanasoshalaiti mashuhuri Zari Hassan amezuru   Uganda  ambako wanahabari wa nchi hiyo wamepata furasa maalum kumuuliza maswali  yanayohusiana na maisha yake.

Zari akizingumza kuhusu mahusiano yake mapya na GK Choppa alieleza kuwa amekuwa akijaribu kumchumbia kwa takriban miaka mitatu ila  juhudi zake zote zilikuwa zinambulia patupu kwani hakuwahi kumpatia nafasi. Lakini kadiri siku zilivyosonga alibadilisha nia na kuanza kumpenda.

"Sikumpa umakini. Lakini baada ya muda, niliamua kukutana naye na nikagundua kuwa ana moyo mzuri. Ni mtu mzuri,” Zari alisema

Vilevile alifafanunua kuhusu uhusiano wake na Diamond Platnumz na kudai kuwa hawajawahi kurudiana ila wana ukaribu mkubwa ikizingatiwa kwa kuwa wao ni wazazi wenza.

"Naapa, hatujalala pamoja kwa muda mrefu, Sisi ni marafiki tu, kwa sasa  nimekua nikimpenda kuliko hata tulipokuwa wapenzim," Zari alisema.