Wahu awashukuru mashabiki wake kwa kumfanya kuwa maarufu

Muhtasari

•Msanii maarufu wa kike Wahu amewashukuru mashabiki wake kwa kuendelea kupenda  kazi zake za muziki na kumfanya kuwa maarufu nchini .

wahu 4
wahu 4

Msanii maarufu wa kike Wahu amewashukuru mashabiki wake kwa kuendelea kupenda  kazi zake za muziki na kumfanya kuwa maarufu nchini .

Mama huyo wa watoto wawili anasema wakati fulani alikuwa na huzuni lakini Wakenya bado walimuunga mkono bila kujua shida alizokuwa akipitia kipindi hicho.

Kupitia ukurusa wake wa Instagram, Wahu alieleza kuwa Machi ni mwezi wake wa kuzaliwa na kukiri kuwa hakuwai fikiria kuwa hatawai kuwa mwanamuziki mashuhuri nchini Kenya. 

"Ni mwezi wangu wa kuzaliwa, si unajua mnajua nasikie vizuri nikikutana na watu ambao wananiambia wamekuwa akinisikiza tangu nilipoanza, nakukiri kuwa nimewagusa kwa namna moja au nyingine. Uaminifu  weyu umenifanya kuendelea kufanya zaidi,mimi sikuwai kuwa na mpango wa kuwa maarufu ila nilikuwa nafanya kazi niliyokuwa nikipenda.”

vilevile alimshukuru  Nameless kwa kuwa baba wa watoto wake na mume wake huku akiri kwamba anampenda jinsi alivyo.