Nandy ashindwa kuvumilia upweke baada ya Billnas kwenda Dubai

Muhtasari

•Wiki jana Billnass alimvisha Nandy pete ya uchumba nyumbani kwao Nandy, huku wakifichua kwamba ndoa rasmi haitopita mwezi wa sita.

The Africa princess 'Nandy'
The Africa princess 'Nandy'
Image: Facebook/ Nandy

Mwanamuziki wa kike Nandy amefunguka makubwa baada kuandika ujumbe  kwenye ukurasa wa mpenziwe kuwa anataka arudi nyumbani haraka.

Mpenzi wa Nandy, Billnass aliondoka nchi ya Tanzania kuekelekea Dubai ambapo inasemekana ameenda kwa shughuli ya kibiashara.

Wiki jana Billnass alimvisha Nandy pete ya uchumba nyumbani kwao Nandy, huku wakifichua kwamba ndoa rasmi haitopita mwezi wa sita.

Billnass alimjibu Nandy kwa kumueleza kuwa anatafuta vazi ambalo atavaa siku ya harusi ambayo inasubiriwa kwa hamu kubwa na Mashabiki wa wiwili hao.

"Nandy nakutafutia gauni la Harusi, Maana hizi vita zinanichanganya tunaweza fungia ndoa kwa kifaru,"alisema Billnas.

Ni hivi majuzi Nandy amekanusha madai kwamba amechepuka baada ya mtangazaji wa shirika la habari nchini humo, kumfumania usiku akisindikizwa kwenye gari na mwanamume mwingine ambaye Mwijaku alibaini si yule ambaye amemchumbia juzi, Billnass.