Harmonize atoa machozi jukwaani, anamtamani ex wake?

Muhtasari

• Msanii maarufu kutoka Tanzania, Harmonize anaonekana anaonekana kuwa na hisia kwa mpenzi wake wa awali, Kajala Frida.

• Baadaye ilimlazima kwenda kimya kwa muda kiasi kabla ya kuimba wimbo mwingine jukwaani.

 

Instagram, KWA HISANI
Instagram, KWA HISANI
Image: Harmonize

Msanii maarufu kutoka Tanzania, Harmonize anaonekana anaonekana kuwa na hisia kwa mpenzi wake wa awali, Kajala Frida.

Hili lilionekana wazi wakati ‘tembo’ alipopanda jukwaani katika hafla yake ya AfroEastCarnivore iliyofanyika mtaani Tabata.

Harmonize alipoanza kuimba wimbo wake wa #Mtaje, alionekana kulemewa na hisia na hata kutoa machozi , kwa kile kilichosemekana kuwa anazipeza enzi za penzi lake na Kajala.

Baadaye ilimlazima kwenda kimya kwa muda kiasi kabla ya kuimba wimbo mwingine jukwaani.

Konde alitoa wimbo huo mahususi kwa minajili ya kumsifia Kajala na kuonyesha ni jinsi gani alikuwa akilithamini penzi lao na kwamba angetaka sana warejeleane na kuzidisha mahaba.

Ifahamike kwamba Harmonize tayari ana mpenzi mwengine kutoka ughaibuni kwa jina Briana, huku wengi wa mashabiki na wadadisi wa burudani huko Bongo wakishuku iwapo penzi hilo litaendelea kama Harmonize atazidi kuonyesha mubashara hisia zake kwa Kajala.

Mpaka sasa bado Frida Kajala hajatangaza iwapo ana mpenzi mpya, huku wengi wakisema hali hiyo inatoa mazingira mazuri kwa wawili hao kurejeleana.