Mtumbuizaji wa Nigeria aliyejibadili kutoka mwanaume kuwa mwanamke ammezea mate Diamond Platnumz

Muhtasari

•Bobrisky ambaye alibadilisha jinsia yake kuwa mwanamke amesifia sana kipaji na sura Diamond huku akisema kuwa angependa kukutana naye hivi karibuni.

Image: INSTAGRAM// DIAMOND PLATNUMZ, BOBRISKY

Mtumbuizaji na mfanyibiashara mashuhuri kutoka Nigeria Idris Okuneye almaarufu Bobrisky ameashiria upendo mkubwa kwa staa wa Bongo Diamond Platnumz.

Bobrisky ambaye alibadilisha jinsia yake kuwa mwanamke amesifia sana kipaji na sura Diamond huku akisema kuwa angependa kukutana naye hivi karibuni.

Licha yake kuwa na asili ya Nigeria, Bobrisky alitumia lugha ya Kiswahili kumwandikia Diamond ujumbe kwenye ukurasa wake wa Instagram.

"Uuwi, Ni mzuri alafu anakipaji kiukweli. Ningependa kukutana na yeye hivi karibuni.. Tanzania nakuja Bongo siwezi kusubiri tena muwe tayari!! @diamondplatnumz," Bobrisky aliandika.

Haya yalijiri baada ya Diamond baada ya Diamond kuacha ujumbe chini ya video ambayo mwanamitindo huyo alipakia Instagram.

Katika video hiyo Bobrisky alionekana akiwa ameshika kifurushi kikubwa cha pesa huku wimbo 'Iyo' ambao Diamond  amewashirikisha Focalistic, Mapara A Jazz na Ntosh Gazi ukiendelea kucheza upande wa nyuma.

Diamond alitaza video hiyo na  kujibu  "Queen Risky đź‘‘" . Aliendelea kuichapisha tena video hiyo ya Bobrisky kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Bobrisky kuona hivyo alitafuta picha ya Diamond na kuipakia kwenye ukurasa wake kisha kuandika ujumbe mtamu kwa msanii huyo chini yake.