Nadia Mukami atarajia mtoto wake wa kwanza

Muhtasari
  • Mapema mwaka huu mcheshi Jalang'o alidai kwamba Nadia ni mjamzito, na kwamba anapaswa kuacha kuficha ujauzito wake
  • Ni matamshi ambayo yaliwagadhabisha wapenzi hao wawili, huku ikimlazimu Jalang'o aombe msamaha
Nadia Mukami na Arrow Bwoy
Nadia Mukami na Arrow Bwoy
Image: hisani

Msanii Nadia Mukami na mpenzi wake Arrow Bwoy, walivuma sana mitandaoni baada ya kutambulisha uhusiano wao kwa wanamitandao.

Mapema mwaka huu mcheshi Jalang'o alidai kwamba Nadia ni mjamzito, na kwamba anapaswa kuacha kuficha ujauzito wake.

Ni matamshi ambayo yaliwagadhabisha wapenzi hao wawili, huku ikimlazimu Jalang'o aombe msamaha.

Habari za ujauzito wake zimeenea sana mitandaoni, huku ujauzito wake ukionekana wakati wa uzinduzi wa Lola and Safari Foundation.

Hata baada ya uvumi kuenea kwamba msanii huyo ana ujauzito hakuthibitisha wala kuzungumzia uvumi huo.

Ni wazi kwamba wapenzi hao wawili wanatarajia kifungua mimba wao.

Awali akijibu madai ya Jalang'o alisema;

"Ulipaswa kuchukua simu yako na kumuuliza Arrow Bwoy... kwa sababu huwezi kujua kwa nini watu hufanya mambo fulani Kama ni ukweli, namaanisha, watu wamekuwa wakizungumza, watu wamekuwa wakitutukana na hatujali kwa sababu mimi na yeye .. tunajua ukweli

Arrow Bwoy hajui vita, aliwapoteza watu wawili maishani mwaka mwaka jana baba yake na Safari," Alizungumza Nadia.