'Unadhani mwanaume ni saizi!' Grand P amtishia msanii aliyejaribu kumpokonya kipenzi chake

Muhtasari

•Miezi mitatu iliyopita mwanamuziki huyo ambaye ana maumbile ya kimbilikimo alitangaza vita na Roga Roga baada yake kuonekana akijiburudisha na mkewe Eudoxie Yao.

•Grand P ambaye anafahamika kuwa tajiri mkubwa ameendelea kusisitiza heshima kutoka kwa Roga Roga.

Grand P na Eudoxie Yao
Grand P na Eudoxie Yao
Image: INSTAGRAM

Mwanamuziki na mwigizaji mashuhuri kutoka Guinea Moussa Sandiana Kaba almaarufu Grand P  amefufua ugomvi wake namsanii mwenzake kutoka Congo, Roga Roga.

Miezi mitatu iliyopita mwanamuziki huyo ambaye ana maumbile ya kimbilikimo alitangaza vita na Roga Roga baada yake kuonekana akijiburudisha na mkewe Eudoxie Yao. Picha za msanii huyo akiwa anajivinjari na Bi Yao ambazo zilikuwa zinaenezwa mitandaoni kwa wakati huo zilimtia hofu Grand P kuwa huenda akapokonywa jiko lake.

Kufuatia hayo Grand P alitoa onyo kali kwa mwanamuziki huyo wa Rhumba Bilionea huyo dhidi ya kuendeleza uhusiano na mkewe.

"Ndugu yangu Roga Roga nakuheshimu sana wewe na watu wote wa Kongo... Lakini  njia unayotaka kufuata si ya kupendeza kwako, usifurahie kuwa karibu na mke wangu la sivyo nitachukua hatua mbaya. Hii ni onyo, Asante!" Grand P alimwambia Roga Roga.

Miezi mitatu baadae, Grand P ambaye anafahamika kuwa tajiri mkubwa ameendelea kusisitiza heshima kutoka kwa Roga Roga.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Grand P amemwambia Roga Roga kuwa licha ya udogo wake ana uwezo zaidi yake.

"Roga Roga wewe ni mdogo kwangu. Unafikiri kweli mwanaume ni saizi?? Unajiona bokoko, mimi nitakugeuza kuwa bokaka!" Grand P alimwambia Roga Roga.

Bilionea huyo aliambatanisha ujumbe wake kwa Roga Roga na kanda ya video inayoonyesha akiwa anapiga tizi katika ukumbi wa mazoezi.

Hivi majuzi Grand P alimvisha mpenzi wake pete la uchumba na kuahidi kufunga ndoa naye hivi karibuni.