Hatupangwi! Diamond apinga kuteuliwa kwa Nyerere kusimamia sanaa

Muhtasari

• Msanii Diamond Platnumz ametofautiana vikali na hatua ya kuteuliwa kwqa muigizaji Steven Nyerere kuwa msemaji wqa wasanii wanamuziki nchini Tanzania.

Image: INSTAGRAM// DIAMOND PLATNUMZ

Msanii Diamond Platnumz ametoa tamko lake kuhusu usimamizi wa muziki nchini Tanzania, muda mchache tu baada ya muigizaji wa bongo movie Steven Nyerere, kuteuliwa na shirikisho la muziki nchini humo kuwa msemaji na bwana mipango wa kuratibu shughuli zote za wasanii nchini humo.

Mwanzo kabisa kwa kukuelewesha tu ni kwamba Nyerere si msanii wa bongo fleva lakini ameteuliwa kuwa msemaji wa wanamuziki, jambo ambalo limezua nyufa kubwa baina ya wasanii hao, baadhi wakimpongeza huku baadhi wakikashfu uteuzi wake.

Fid-Q ambaye ni msanii mkongwe kwenye game la bongo fleva amekuwa mstari wa mbele kumpongeza na kutetea uteuzi wa Nyerere huku wanamuziki wengi wakiupinga vikali, akiwemo mfalme wa muziki Diamond Platnumz.

“Serikali ina nia njema sana ya kukuza Sanaa, ila inatakiwa kuwa makini sanaq na watu wanaoteuliwa kusimamia Nyanja mbalimbali katika tasnia zetu, maana watu hao wanachokifanya ni kulidhalilisha taifa na kulifanya taifa letu lionekane halina weledi,” aliandika Diamond kwenye instastories zake.

Pia Diamond hakusita kumjibu msanii Fid-Q na kumtaka aache kujidhalilisha kwa kumpongeza mtu tu kama kipofu bila kujali.

“Fid-Q mbele ya kamera unatabasamu ila najua kabisa ukikaa peke yako unajuta na kujua kuwa umejivunjia heshima kubwa ulioijenga kwa muda mrefu. Wewe ni ICON usikubali kupoteza legacy uliyoijenga kwa maumivu na jasho, kisa tu mihemko pasi na kutumia fikra,” Simba alinguruma kupitia instastories zake.