“Mungu akulinde binti yangu mrembo” Vera Sidika aadhimidha miezi 5 tangu kuzaliwa kwa bintiye

Muhtasari

•Vera alimtakia binti yake ulinzi wa Maulana huku akimhakikishia kuhusu upendo wake mkubwa kwake.

Image: INSTAGRAM// VERA SIDIKA

Binti wa pekee wa mwanasoshalaiti Vera Sidika, Asia Brown alitimiza miezi mitano siku ya Jumapili.

Vera alichukua fursa hiyo kusherekea ukuaji wa binti huyo wake ambaye alikaribishwa ulimwenguni mnamo Oktoba 20, 2021.

Katika ujumbe wake, mke huyo wa mwanamuziki Brown Mauzo alimtakia binti yao ulinzi wa Maulana huku akimhakikishia kuhusu upendo wake mkubwa kwake.

"Siwezi kuamini siku nyingine tu Asia Brown alikuwa ndani ya tumbo langu. Mungu akulinde daima binti yangu mrembo. Nakupenda sana," Vera aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Mwanasoshalaiti huyo mwenye umri wa miaka 32 alimtaja Asia Brown kama rafiki yake mkubwa zaidi. Alisema kwamba anatamani sana bintiye akue haraka.