Dadake Diamond, Esma Platnumz afunguka kuhusu mahusiano yake

Muhtasari

•Mama huyo wa watoto wawili alisema kwamba yupo tayari kuongeza familia na mpenzi wake wa sasa asiyetambulishwa.

•Mnamo Julai 2020, Esma aliolewa kama mke wa tatu na mfanyibiashara wa Tanzania Yahya Msizwa.

Esma Platnumz na Diamond Platnumz
Esma Platnumz na Diamond Platnumz
Image: HISANI

Dadake Diamond, Esma Platnumz amefichua kwamba yupo kwenye mahusiano.

Akizungumza na wanahabari katika hafla ya uzinduzi wa video za EP ya FOA, Esma hata hivyo alisema kwamba kwa sasa ameamua kuficha mahusiano yake.

"Niko kwenye mahusiano. Lakini mahusiano yangu sio ya kujionyesha kama zamani. Ni mahusiano ambayo tukikutana tunaburudika tu," Alisema Esma.

Mama huyo wa watoto wawili alisema kwamba yupo tayari kuongeza familia na mpenzi wake wa sasa asiyetambulishwa.

Esma hata hivyo aliweka wazi kwamba bado hajawazia suala la kufunga pingu za maisha naye.

"Mahusiano yangu kwa sasa ni siri. Sifikiri ndoa. Bado sana. Ikitokea tunaweza kuongeza familia. Ila kwa sasa bado," Alisema.

Alifichua kwamba mpenzi wake pia alikuwepo kwenye hafla hiyo ya uzinduzi wa video za EP ya kakake.

Mnamo Julai 2020, Esma aliolewa kama mke wa tatu na mfanyibiashara wa Tanzania Yahya Msizwa.

Hata hivyo, takriban miezi mitatu baadae alifichua kwamba ndoa yao ilikuwa imegonga ukuta.