Thee Pluto abadilisha muonekano kwa kukata 'rastas' zake

Muhtasari

• Thee Pluto amebadilisha muonekano wake kwa kunyoa rasta.

Thee Pluto
Thee Pluto
Image: INSTAGRAM

Mwanablogu mwenye ushawishi mkubwa kupitia mtandao wa YouTube, Thee Pluto hatimaye amebadilisha muonekano wake kwa kunyoa ‘rasta’ zake ndefu ambazo kwa muda mrefu zimekuwa kama nembo yake ya utambulisho.

Thee Pluto ambaye alipata umaarufu mkubwa baada ya kuanzisha kipindi kwenye mitandao kwa jina la Loyalty Test amewaacha wengi wakizungumza huku akiwa hajatoa sababu yoyote ya kunyoa nywele zake.

Wengi walihisi ni njia moja ya kujaribu kuwazuga wazazi wa mpenzi wake kumkubalia kama mkazamwana katika familia, kutokana na maneno aliyoyaweka wazi hivi majuzi kwamba yeye na mpenzi wake hawapo karibu kabisa na kuachana.

Itakumbukwa familia nyingi za Kiafrika huwa wanachukulia mtu mwenye rasta kama mtu mhuni ambaye hajatulia katika utu uzima wa sinia la mapenzi na pia nywele hizo huusishwa pakubwa na watu wasiowajibika katika jamii.

Thee Pluto alipakia picha zake akiwa ameshikilia nywele hizo alizozinyoa mikononi na kusema tu kwamba amerudi kuonekana kama mtoto tena.

“Ati nimekuwa kama mtoto tena, mko na ufala,” aliandika Pluto kuwasuta wale waliokuwa wakisema muonekano wake umemtoa kama kijana ambaye bado hajabaleghe.