Diana Marua: Kupendwa na mtu wa maana ni zaidi ya kila kitu

Muhtasari

• Kupendwa na mtu ambaye ana umuhimu mkubwa maishani ni zaidi ya kila kitu - Diana Marua kwa Bahati.

Bahati na mpenzi wake Diana Marua
Bahati na mpenzi wake Diana Marua
Image: INSTAGRAM

Diana Marua amechukua kwenye mtandao wa Instagram na kuachia ujumbe mmoja mfupi lakini matata kwelikweli akimsifia mumewe Bahati kwa mapenzi mubashara yasiyojua mwisho ni kumaanisha nini.

Wapenzi hao wawili wanajulikana kwa kuanika kila hatua ya maisha yao yote kutoka mapenzi hadi biashara kwenye mitandao ya kijamii bila woga wala kutetereka.

Marua amemsifia Bahati na kusema kwamba siku zote anahisi amependwqa na mtu ambaye ni wa muhimu sana katika maisha yake.

Aisee, mapenzi na urafiki vikikutana, basi kifo ndio muamuzi wa utengano!

“Kupendwa na mtu ambaye ana umuhimu mkubwa maishani ni zaidi ya kila kitu,” aliandika Marua akiambatanisha ujumbe huu kwa picha moja kali wakiwa wanarushiana tabasamu la geresha na mumewe, Bahati.

Hivi majuzi wakati Bahati alitangaza kujiunga na chama cha Jubilee ili kuwania ubunge wa Mathare katika uchaguzi mkuu wa Agosti, Diana aliikaribisha hatua hiyo na hata kuweka wazi kwamba atamsaidia kadri ya uwezo wake mpaka aingie bungeni.

Wiki hii wawili hao wamewakosha mahasidi waliokuwa wakiwasema baada ya kuhamia kwenye nyumba ambayo walinunua kama zawadi ya Valentino mnamo mwezi Februari.

Hatua hiyo ilizima midomo moto ya wambeya waliokuwa wakisambaza habari kwamba nyumba hiyo si yao bali walikodisha kwa muda kwa ajili ya mbwembwe tu za mitandaoni kama ilivyo kawaida yao.