Huddah Monroe: Shukrani kwa kunisapoti licha ya kujifungia kutoka kwenu

Muhtasari

Watu wanadhani kuwa nina madharau na kebehi lakini si kweli. Nina wasiwasi wa kijamii. - Huddah Monroe

Huddah Monroe
Huddah Monroe
Image: instagram

Huddah Monroe ni mwanamitindo na mwanasosholaiti ambaye ni kipenzi cha wengi kutokana na jinsi anavyojibeba na brand yake.

Pia ni mjasiriamali wa vipodozi ambaye kwa kweli kina dada wengi wanamtazamia kama kioo cha jamii.

Lakini miezi ya hivi karibuni mwanadada huyu amekuwa akionekana sana kujuta kuwa maarufu na kuchukuliwa kama kioo cha jamii na wengi.

Baada ya kudokeza sababu zake za kujuta kuwa maarufu na pia kuonekana akiadimika sana mitandaoni, Huddah hata hivyo amewashukuru sana wafuasi na mashabiki wake ambao wanazidi kumuaminia na kuyakubali maamuzi yake ya kuadimika katika video za mitandaoni.

Amefichua kwamba japo wengi wanadhani ni maringo lakini ana tatizo kubwa analipigana ambalo ni wasiwasi wa mitandao ya kijamii.

Awali, Huddah alisema kwamba tatizo hili lilitokana na watu aliokuwa na ukaribu nao akiwachukulia kama marafiki wa kufa kuzikana, baadae kumgeuka na kumsaliti, hatua iliyompelekea kupoteza Imani yake kwa watu wote.

Tatizo hilo kulingana na yeye linamsababishia mpaka ana woga wa kupanga mtoko na Rafiki zake au hata kukutana tu na kubarizi. Amewashukuru wote wanaomuelewa hata kama anaonekana kujifungia sana.

“Nawapenda nyinyi nyote kwa kunisapoti licha ya kuonekana kama nimejitenga na kujifungia sana. Watu wanadhani kuwa nina madharau na kebehi lakini si kweli. Nina wasiwasi wa kijamii. Hili linaniogofya hata kupanga ‘date’ na Rafiki zangu au hata ku-link up. Na mnaweza gundua hilo kutokana jinsi nimekuwa adimu katika mazungumzo ya video,” aliandika Huddah.