Huddah: Naogopa kutangamana, rafiki zangu waliniwekea sumu

Muhtasari

• Mimi nilikuwa msichana ambaye ningekuwa na wasichana wenzangu kama 20 hivi kwenye nyumba yangu tukitafuna miraa, kunywa na kutumia dawa. Wote walinisaliti na wengine hata wakaniwekea sumu - Huddah Monroe.

Mwanasosholaiti Huddah Monroe
Mwanasosholaiti Huddah Monroe
Image: INSTAGRAM

Mjasiriamali na mwanasosholaiti Huddah Monroe hatimaye ameweka wazi kuhusu kubadilika kwa tabia yake mitandaoni katika miaka ya hivi karibuni.

Huddah anasema kwamba amebadilisha jinsi alivyokuwa akifanya mambo mengi sana awali kutokana na kuwa na wasiwasi wa mitandao ya kijamii, jambo ambalo limemfanya kufanya mambo yake mengi mbali sana na kamera za mapaparazi.

Mwanamama huyo amefichua kwamba kubadilika ghafla kwa tabia yake hiyo kunatokana kwamba Rafiki zake wengi ambao walikuwa wanakula naye walimsaliti na baadhi kujaribu kumwekea sumu.

Huddah amefichua kwamba siku hata hataki tena kuwa karibu na watu na hata wale wachache ambao ni marafiki zake hawajui anaishi wapi kutokana na woga wa kuogopa kufanyiwa kama marafiki wa awali walimfanyia.

Unaambiwa aliyeumwa na nyoka hata akiona Kamba lazima atatetereka aisee!

“Mimi nilikuwa msichana ambaye ningekuwa na wasichana wenzangu kama 20 hivi kwenye nyumba yangu tukitafuna miraa, kunywa na kutumia dawa. Wote walinisaliti na wengine hata wakaniwekea sumu. Nina woga sana hata kumuamini mtu yeyote mpaka kufikia kiwango kile. Rafiki zangu hata hawajui ninakaa wapi. Huwa sialiki mtu yeyote kuja kwa nyumba yangu na wala sijawahi enda katika nyumba za watu. Kwa sababu ninaogopa kumkubalia mtu yeyote kuwa karibu na mimi,” aliandika Huddah kwenye instastories zake.