Wafrika wanadunishwa! - Huddah atoa sababu ya kutojihusisha na Young Famous & African

Muhtasari

• Huddah ametoa sababu zake za kutojihusisha na kipindi cha Netflix, Young Famous & African

• Wafrika wanadunishwa na kupewa malipo ya chini kwa sababu tunapenda umaarufu sana kuliko hata kuutengeneza - Huddah

Mwanamitindo Huddah Monroe
Mwanamitindo Huddah Monroe
Image: INSTAGRAM

Mwanamitindo wa muda mrefu Huddah Monroe baada ya kutajwa na wakenya wengi kama mtu ambaye alistahili pakubwa kushirikishwa katika kipindi halisia cha Netflix, Young Famous and African, hatimaye amevunja kimya chake kuhusu kutotaka kushiriki hata kama angepewa mwaliko.

Huddah akitolea mfano wa kipindi kama hicho kwenye Netflix kinachofanywa na staa wa hiphop kutoka Marekani, Kanye West, alisema kwamba Wafrika wanadunishwa katika malipo na ndio sababu kuu ya kutovutiwa nacho.

Kulingana na Huddh, Kanye West analipwa kima cha $30 milioni ambacho ni kiasi sawa na trilioni 3 na upuzi pesa za Kenya, alisema kwamba ana uhakika Wafrika wote wanaoshiriki katika kipindi hicho hawawezi kulipwa kiasi hicho na pia akasema anatamani sana kujua wanalipwa kwa kiwango kipi.

“Wafrika wanadunishwa na kupewa malipo ya chini kwa sababu tunapenda umaarufu sana kuliko hata kuutengeneza. Ninatamani kujua wanalipwa aje. Nimeona watu wengi wakini-tag kuhusu YFA lakini sijaiangalia kwa sababu nipo katika likizo,” aliandika Huddah kwenye instastories zake.

Maana yake kubwa ni vkwamba Wafrika wanapenda sana vitu vya bwerere ilimradi tu wajulikane na kuwa maarufu bila hata kutia juhudi katika kuutafuta umaarufu huo kwa jasho.