S2Kizzy kufanya 'project' na Rihanna? aandika na kufuta

Muhtasari

• Producer S2Kizzy aliwachanganya wengi baada ya kuachia ujumbe kwamba atakuwa mtu wa kwanza kufanya project na msanii Rihanna na kisha baadae kuhariri kwa kutoa jina la Rihanna.

S2Kizzy na Rihanna
S2Kizzy na Rihanna

Mzalishaji matata wa ngoma za bongo fleva, S2kizzy ameachia ujumbe usioeleweka kwenye Instagram yake ambapo alitamba kwamba yeye ndiye mtu wa kwanza kuwahi kutokea kutoka ukanda wa Afrika mashariki kushiriki katika mradi mmoja na staa kutoka Barbados, Rihanna.

Producer huyo baadaye alihariri ujumbe huo na kutoa jina la Rihanna ambapo aliweka emoji za mduara wa dunia badala yake, na hili limewatatanisha watu wengi kushindwa kuelewa alichokuwa akimaanishi awali kwa kuweka jina la Rihanna.

“Mtu wa kwanza kutoka Afrika mashariki kuwa katika kazi ya msanii Rihanna,” ujumbe wa kwanza kabla kuhariri ulisoma.

“Mtu wa kwanza kutoka Afrika Mashariki kuwa katika mradi wa 🌏🌍🌍🌎,” ujumbe wa pili baada ya kuhariri ulisoma.

Baada ya kuliondoa jina la Rihanna kwenye post yake hiyo, wengi wamesema labda ni kiki tu alikuwa anatafuta kwa kujizolea uhodari kwa kuwa wengi wanamjua Rihanna kama msanii wa kimataifa anayetamba mno.

Je, wewe unahisi S2kizzy alikuwa anamaanisha nini awali kusema ako katika ‘project’ ya Rihanna na kisha baadae kulitoa jina la staa huyo wa kimataifa?