Mapenzi kikohozi! Zari anengua maungo kwa kibao kipya cha Diamond

Muhtasari

•Zari alisikika akiucheza wimbo namba mbili kwenye albamu ya FOA, 'Somebody' ndani ya gari lake.

Mwanasoshalaiti na mfanyibiashara mashuhuri kutoka Uganda, Zari Hassan ameonekana kuvutiwa na EP mpya ya aliyekuwa mumewe, Diamond Platnumz. 

Katika kanda ya video ambayo alipakia Instagram, Zari alisikika akiucheza wimbo namba mbili kwenye albamu ya FOA, 'Somebody' ndani ya gari lake. 

Mama huyo wa watoto watano alionekana akisakata densi huku wimbo huo wa kimapenzi wa Diamond ukiendelea kucheza.

Image: INSTAGRAM// ZARI HASSAN

Zari ambaye ana watoto wawili na Diamond alionekana kufahamu vizuri maneno ya wimbo huo kwani pia yeye alikuwa akiuimba ulipokuwa unaendelea.