Pritty Vishy alalamika kunyang'anywa Stivo Simple Boy na Adasa

Muhtasari

• Pritty Vishy, mpenzi wa Stivo Simple Boy analia kwamba ameachwa na msanii huyo ambaye anasema ameendea mwanamuziki mwenza kwa jina Adasa.

Pritty Vishy, Stivo Simple Boy
Pritty Vishy, Stivo Simple Boy
Image: INSTAGRAM

Mpenzi wa msanii Stivo Simple Boy, Pritty Vishy Jumatatu amepakia video kwenye Instagram yake akilia kwa kile alisema kwamba mchumba wake huyo amemuacha kwa ajili ya mwanamke mwingine.

Katika video hiyo, Vishy anasikika akiteta kwamba Stivo amemuacha kwa ajili ya mwanadada mwingine kwa jina Adasa, ila haijajulikana wazi kama ni Adasa yule mmoja mwanamuziki ama ni mwingine anayetumia jina na picha yake.

Kwenye mabishano picha zilizopakiwa Instagram, Adasa wanaonekana na Stivo ambapo Pritty Vishy anaachia ujumbe mzito akimpasha mwanadada huyo kwa kumchukulia mchumba.

Mwanablogu huyo chipukizi analia akijuta kwa yale mengi ambayo amemfanyia Stivo Simple Boy lakini baadae akamchorea nje.

“Stivo mbona unanifanyia hivi, nilifanya mambo mengi kwa ajili yako, nilijitoa mhanga pakubwa, mbona Adasa? Ina maana yeye ni mrembo kuniliko? Anakufaa? Mbona unachagua mwanamke mwingine kuniliko, ana nini ambacho mimi sina” anasikika akizungumza katikati ya kwikwi.

Katika majibizano ya Vishy na Adasa kwenye, wawili hao wanaonekana wakitupiana maneno kimzaha tu, jambo ambalo limefanya wengi kuamini kwamba Stivo hajamuacha Vishy kwa ajili ya Adasa bali ni kiki tu wanajaribu kuigiza.

Ikumbukwe waqsanii na watu maarufu wengi ndani na nje ya nchi wamekuwa na mazoea ya kufanya mambo ya ajabu kwacajili ya kiki tu.

Hivi majuzi msanii mkubwa kutoka Tanzania, Nandy alifanya kufuru kubwa baada ya kutafuta kiki kwa kudai kwamba wameachana na mchumba wake Billnass, ila siku moja baadae ikaja kugundulika kwamba alikuwa anafukuzia kiki ili kupata umakini wa wafuasi wake kwa ajili ya kibao chake kipya ambacho alikiachia baadae siku hiyo.